Pata Habari kwa kuandika email yako hapa chini:

Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

hii ndiyo skendo mpya inayomnyima usingizi justine bieber...!

0 comments

justin-bieber-madison-beer-studio

Akiwa mtoto msanii mdogo tu, na msanii marufu kwa kipindi hiko Justine Bieber alishtumiwa kwa kutukana ngozi nyeusi na hivyo kuwakera sana raia wengi wa nchini marekani, video hiyo iliyokuwa ikifichwa kutonekana na mtu yoyote, ilifikia uma ikionyesha Justine akisema kuwa watu weusi wanaogopa mmisumeno ya umeme, huku akiwa anafanya kama utani hivi, skendo hiyo imeibuliwa tena hivi majuzi na kutokea watu wengi kumuandama justine Bieber kwa kitendo hicho alichowahi kufanya akiwa na umri mdogo tu wa miaka 15, kutokana na kusemwa sana Justine Bieber kuonyesha kuw amebadilika sasa na amekua mtu mzima, akaona isiwe ishu na kuamua kuomb msamaa kwa mara nyingine.
Skendo za ubaguzi wa Rangi nyeusi zimeonekana kushika hatamu hivi karibuni, watu maarufu wengi kuonekana kuchukizwa na vitendo hivyo hata kama bado wao wana ngozi nyeupe, kitendo hiko kwa hivi sas kimetokea kuchukiza kila aina ya raia, vitendo vya ubaguzi w rngi vimeendelea kushika kila sehemu, kuanzia sector ya burudani hadi michezo.

Kumbe mume wa mjamzito aliyepigwa mawe Pakistan alimuua mke wake wa kwanza..!

0 comments
Screen Shot 2014-05-30 at 6.18.22 PMMume wa Farzana Parveen ambaeni mwanamke mjamzito wa Pakistan aliepigwa mawe hadi kufa kutokana na kuamua kuolewa na Mwanaume anaempenda kinyume na pendekezo la familia la kutaka aolewe na mwanaume wanaemtaka wao, amekiri kufanya mauaji ya mke wa kwanza kabla ya Farzana na kusema alifanya hivyo ili aweze kufunga ndoa na Parveen
Mwanaume huyo Mohammad Iqbal amesema alitaka kuwasilisha maombi yake kwa Parveen hivyo aliamua kumuua mke wake kwanza ambapo mamlaka za nchini Pakistan zimesema ni kweli Mwanamke huyo wa kwanza aliuwawa miaka sita iliyopita.
Baaday a mauaji Iqbal alikamatwa na polisi na baadae kuachiwa kwa dhamana kwasababu mtoto wake wa kiume alimsamehe kutokana na kitendo hicho.
mjamzitoMtoto wake ambaye kwa wakati huo alikuwa na umri wa miaka 20, amethibitisha taarifa hizo na kusema baba yake alitumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani kutokana na mauji hayo.
Parveen ambae ndio mke wa pili baada ya wa kwanza kuuwawa, alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu na alipigwa mawe hadi kufa na kundi la watu wakiwemo kaka zake, baba yake mzazi na ndugu wa familia yake Mashariki mwa mji wa Lahore kwa sababu aliamua kuolewa na Mwanaume ambae familia yake haikua inamtaka.
Tayari waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif amemtaka waziri wa Jimbo hilo kuwasilisha maelezo juu ya tukio hilo la Mwanamke huyu kuuwawa na ujauzito wake.

MELI YA MJAPANI ILIYOUNGUA BAHARIN..!

0 comments
Screen Shot 2014-05-30 at 11.57.11 AMMlipuko mkubwa umetokea kwenye meli kubwa ya mafuta nchini Japan katika Pwani ya Kusini Magharibi mwa bandari ya Himeji na kusababisha mtu mmoja kati ya wanane waliokuwa ndani ya meli hiyo kupotea huku wengine wanne wakijeruhiwa vibaya.
Moto mkubwa ulilipuka katikati ya bahari ambapo meli hiyo yenye uzito wa tani 998 iliyokuwa ikitokea mji wa Hiroshima kuachwa ikielea ndani ya maji baada ya ajali hiyo na baadae kufatwa na meli za kupambana na majanga ya moto.
Screen Shot 2014-05-30 at 11.57.46 AM
Watu saba wameokolewa katika ajali hiyo mbaya, wanne wakiuguza majeraha ya moto kwa mujibu wa shirika la habari la NHK, ambapo kapteni wa meli hiyo amesema uchunguzi kumtafuta mtu mmoja aliyepotea bado unaendelea.
Screen Shot 2014-05-30 at 11.57.52 AM
Afisa usalama katika Pwani hiyo Koji Takarada amesema chanzo cha mlipuko huo bado hakijajulikana ambapo shirika la habari NHK limeripoti kuwa wafanyakazi wa meli hiyo walikuwa wakifanya kazi chini ya meli wakati mlipuko unatoke.

MMH..HAKUNAGA...KUTANA NA BINTI MREMBO WA RAIS KAGAME WA RWANDA...NI SHIDAAA...!

0 comments
Anaitwa Ange Kagame, ni mtoto wa pili na wakike pekee wa Rais wa 6 wa Rwanda Paul Kagame, mama yake anaitwa Jeannette Nyiramongi na ndiye first lady wa Rwanda.
Ange hajalelewa nchini Rwanda, ameishi maisha yake yote nje ya nchi. Wanafunzi waliosoma naye wanasema binti huyu anajituma sana kwenye masomo na kusaidia watu na muda mwingi hutumia kufuatilia mambo yanayoendelea nyumbani kwao Rwanda.
Kwa sasa Ange amerudi Rwanda na anafanya kazi nyingi za kujitolea kwa jamii kama kuoanda miti, kampeni za kupiga vita magonjwa nguli Rwanda na kuendesha makundi ya kukomboa wanawake kutoka kwenye umasikini.






Ange na kaka'ake Ivan





MADUKA YA WATANZANIA SOUTH AFRICA YACHOMWA MOTO-WADAIWA KUUZA UNGA..!

0 comments
Afrika Kusini ni nchi yenye uchumi mkubwa Afrika ambao umevutia Waafrika wengi kukimbilia huko kwa ajili ya kufanya kazi kama za Udereva, uuzaji mafuta kwenye vituo vya mafuta pamoja na kazi nyingine mbalimbali.
Taarifa kutoka kwenye mji wa Pretoria ni kwamba Watanzania ambao wanamiliki na kufanya biashara mbalimbali zikiwemo za Maduka na wale wanaomiliki hoteli, wamevamiwa wakiwa kwenye mali zao na kufanyiwa uharibifu na nyingine kuchomwa moto.
Ni kundi la watu ambalo linaendeleza uvamizi huu ambapo linawashutumu Watanzania hawa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, yani kwa ufupi Watanzania wanasema hata kama kweli wangekua wanafanya hii biashara, walio na mamlaka ya kuwavamia ni Polisi na sio hao raia.

Inaaminika kundi hili lina sehemu kubwa ya madereva Taxi wazawa wa nchi hiyo ambao wamekua wakiumizwa na jitihada za raia wa kigeni wa Nigeria na Watanzania ambao wamejazana kwenye mtaa wao wakimiliki maduka mbalimbali yakiwemo ya nguo pamoja na hoteli.
Tayari balozi wa Tanzania amekutana na Watanzania hao na kuahidi kulifatilia ambapo ni Watanzania watano wamejeruhiwa wakiwemo watatu ambao bado wako hospitali na mmoja wao kavunjika mkono, mmoja kapigwa kichwani.
Kabla ya Watanzania wengine kuwahi kufunga maduka yao, maduka matatu ya Watanzania pamoja na hoteli mbili zinazomilikiwa na Watanzania zilivamiwa na wakachuchukuliwa simu na watu kupigwa ambapo polisi walipokuja hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya maelezo.
Picha hizi zote zilipigwa na Mtanzania akiwa anakimbia baada ya kufanikiwa kufuduka

Baada ya kutekwa wasichana na Boko haramu Huu ni msaada uliotoka Marekani kwenda Nigeria.!!!

0 comments

obamaNchi ya Marekani imetangaza kutuma kikosi cha wataalamu nchini Nigeria kusaidia kuwatafuta wasichana zaidi ya 200 wa shule waliotekwa nyara mwezi uliopita na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Rais Barack Obama ameshutumu utekaji nyara wa wasichana hao na kusema kuwa mataifa yanapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kulikomesha Boko Haram.
Rais Obama amesema>>”Tayari tumetuma kundi letu,Nigeria wamekubali msaada wetu ambao unashirikisha wanajeshi,wadumishaji wa sheria na mashirika mengine ambao wanajaribu kutambua waliko wasichana hawa ili wawape msaada’.
Rais Obama amesema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kutumia utekeji wa kikatili wa wasichana hao kama msingi wa kuungana na kuangamiza Boko Haram.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amekubali msaada huo kama alivyosema msemaji wake Daktari Reuben Abati>>”msaada huo kutoka kwa Rais Obama uliwasilishwa na Waziri wa Mashauri ya Kigeni John Kerry kama saa tisa alasiri hivi’.
Source:Bbc.