Kumbe mume wa mjamzito aliyepigwa mawe Pakistan alimuua mke wake wa kwanza..!

Mwanaume huyo Mohammad Iqbal amesema alitaka kuwasilisha maombi yake kwa Parveen hivyo aliamua kumuua mke wake kwanza ambapo mamlaka za nchini Pakistan zimesema ni kweli Mwanamke huyo wa kwanza aliuwawa miaka sita iliyopita.
Baaday a mauaji Iqbal alikamatwa na polisi na baadae kuachiwa kwa dhamana kwasababu mtoto wake wa kiume alimsamehe kutokana na kitendo hicho.

Parveen ambae ndio mke wa pili baada ya wa kwanza kuuwawa, alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu na alipigwa mawe hadi kufa na kundi la watu wakiwemo kaka zake, baba yake mzazi na ndugu wa familia yake Mashariki mwa mji wa Lahore kwa sababu aliamua kuolewa na Mwanaume ambae familia yake haikua inamtaka.
Tayari waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif amemtaka waziri wa Jimbo hilo kuwasilisha maelezo juu ya tukio hilo la Mwanamke huyu kuuwawa na ujauzito wake.
0 comments: