Pata Habari kwa kuandika email yako hapa chini:

Baada ya kutekwa wasichana na Boko haramu Huu ni msaada uliotoka Marekani kwenda Nigeria.!!!


obamaNchi ya Marekani imetangaza kutuma kikosi cha wataalamu nchini Nigeria kusaidia kuwatafuta wasichana zaidi ya 200 wa shule waliotekwa nyara mwezi uliopita na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Rais Barack Obama ameshutumu utekaji nyara wa wasichana hao na kusema kuwa mataifa yanapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kulikomesha Boko Haram.
Rais Obama amesema>>”Tayari tumetuma kundi letu,Nigeria wamekubali msaada wetu ambao unashirikisha wanajeshi,wadumishaji wa sheria na mashirika mengine ambao wanajaribu kutambua waliko wasichana hawa ili wawape msaada’.
Rais Obama amesema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kutumia utekeji wa kikatili wa wasichana hao kama msingi wa kuungana na kuangamiza Boko Haram.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amekubali msaada huo kama alivyosema msemaji wake Daktari Reuben Abati>>”msaada huo kutoka kwa Rais Obama uliwasilishwa na Waziri wa Mashauri ya Kigeni John Kerry kama saa tisa alasiri hivi’.
Source:Bbc.

0 comments: