Pata Habari kwa kuandika email yako hapa chini:

Showing posts with label DIAMOND. Show all posts

Exclusive: Pesa iliyotumika kwenye video mpya ya Diamond na Iyanya London, kolabo na Davido tena?

0 comments
Screen Shot 2014-05-27 at 1.31.14 AMWiki iliyopita Diamond Platnumz alikua London Uingereza kwa ajili ya kufanya show lakini pia vilevile kufanya video ya wimbo wake aliofanya na msanii Iyanya wa Nigeria.
AyoTV na millardayo.com zimepata Exclusive interview na meneja Babtale ambae anasimamia kazi za Diamond sasa hivi ambapo amesema kutokana na kupiga hatua kwa Diamond na kuingia kwenye levo za kimataifa, imebidi waanze kufanya video za kiwango hicho cha kimataifa lakini haimaanishi kwamba ndio Platnumz hatofanya tena video Tanzania’
Namkariri Tale akisema ‘video tuliyofanya na Iyanya Uingereza ni kwa sababu tulikua tunamuhitaji Director MoE Musa ambae anaishi na kufanya kazi zake Uingereza ndio maana tukasafiri mpaka huko, kuna video ambayo tutafanya Nigeria tukishatoka Ghana na pia ikitokea kwamba tunatakiwa kufanya video Tanzania tutafanya hivyo’
Screen Shot 2014-05-29 at 2.28.04 AMAyoTV: Mmetumia kiasi gani cha pesa kufanya hii video Uingereza?
Bab Tale: ‘kiukweli tunaumia, tunaumia kwa sababu kumlipa Moe Musa na kupata kila kitu kama kwenye hii video ya juzi tumemlipa Moe peke yake dola elfu 25 ambazo zinagonga mpaka milioni 40 za Kitanzania, bado usisahau tumewatoa kina Iyanya Nigeria kwa hela yetu kuwaleta London, kuwalipia nauli ya business class kwenye ndege na hoteli hawawezi kulala hoteli mbaya kama sisi watoto wa Manzese’

Diamond na Ommy Dimpoz London. (Pichaz na video)

0 comments
Screen Shot 2014-05-19 at 8.13.34 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 8.27.36 AMDiamond alikwenda Uingereza kwa ajili ya kufanya video ya wimbo wake na Iyanya ambayo imegharimu zaidi ya dola za kimarekani elfu 20 (zaidi ya milioni 30 za Tanzania) kutokana na ukubwa wa director wenyewe, malazi, mavazi, kusafirisha watu kutoka Nigeria pamoja na mahitaji mengine.
Baada ya kazi Diamond pamoja na mshkaji wake Ommy Dimpoz wameshea baadhi ya picha zao wakiwa kwenye mitaa mbalimbali ya London Uingereza pamoja na video ya show waliyofanya pamoja London.
Screen Shot 2014-05-19 at 8.14.04 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 8.14.14 AM
Screen Shot 2014-05-19 at 8.24.05 AM



Screen Shot 2014-05-19 at 8.24.14 AM

DIAMOND TNA!!! Dakika 21 za alichokifanya Diamond kwenye MTV Road to mama Club Bilicanas Mei 16..!!!

0 comments
Screen Shot 2014-05-19 at 12.17.38 AMHii ni party ya MTV road to Mama Awards 2014 iliyofanyika Club Bilicanas usiku wa kuamkia May 17 ambapo ndani ya party hii kulikua na watu tofauti kuanzia wanasiasa, wasanii wa filamu na Wanamuziki.
Miongoni mwa watu waliomiliki stage ni pamoja na Diamond ambae hapa kuna video yake jinsi alivyokua kazini… pia vilevile usisahau kumpigia kura kwenye tuzo za MTV Mama kwa kuingia kwenye mtvbase.com

Cheki walichokiandika mastar kadhaa wa Tanzania baada ya Diamond kutangazwa kushiriki kwenye BET!

0 comments
BET-DIAMOND-PLATNUMZ-2014Hii ni Tanzania ambayo kwa sasa Diamond Platnumz ameamua kutuonyesha kwenye ramani ya Dunia,imekua ni good news kwa Tanzania na afrika mashariki kwa ujumla,baadhi ya mastar wa Tanzania wamekubali kutoa ya moyoni baada ya taarifa hiyo miongoni mwao ni pamoja na Mkubwa Fela,Wema Sepetu,Ay,Belle 9,Vanesa Mdee na wengine kibao.
Hizi ndizo post za mastar hawa.

Read More »

BAADA YA KUCHUKUA TUZO 7 ZA KTMA :HII NDIO KAULI YA KWANZA YA DIAMOND KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

0 comments
Hakika ilikuwa ni kazi ngumu sana lakini kwa uwezo wa mwenyez mungu ametufanyia wepesi na hatimaye kufanikisha... Nawashkuru sanasana Mashabiki zangu wote kwakuwa nyie ndio mlionipa tuzo hizi kupitia kura zenu... Family, uongozi wangu.. bila kuvisahau vyombo vyote vya habari vilivyo fanya kazi zangu zisikike kila kona... Niwashkuru pia wasanii wenzangu, kwakuwa naamini wote walifanya kazi nzuri na ndiomaana wote tukawa pale ila kwakuwa mshindi ni mmoja, ikatokea kuwa bahati yangu...Ahsanteni sana, cha mwisho nnachoweza kusema tu ni kwamba (Tika! Tika!) yaani (Saba saba) Nomination 7 Tunzo 7...! tuhamieni MTV Awards tuilete Heshima nyumbani sasa