Pata Habari kwa kuandika email yako hapa chini:

WANAUME WAMENIPOTEZEA MUDA!!!


MNENGUAJI wa Bendi ya FM Academia, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ amesema hahitaji mwanaume yoyote kwa sasa kwani wanampotezea muda kwa kipindi kirefu.
Akizungumza na Centre Spread Queen alisema wanaume wamekuwa wakimsumbua mara kwa mara kutaka kampani ya kimapenzi lakini wengi wao wanakuwa hawana mapenzi ya kweli hivyo anaona bora kuwapiga chini. “Bora niwe singo natafuta pesa kuwazawaza hawa wanaume nitaishia kuumia tu na kushindwa kufanya shughuli zang, tena waache kunifuatafuata kwa sasa,’’ alisema Queen Suzy. Mnenguaji huyo alishawahi kuwa na uhusiano na mwimbaji wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Kalala Junior ambaye alizaa naye mtoto mmoja baadaye akatembea na rapa wa FM Academia, G 7 ambao wote ameshamwagana nao.

0 comments: