Pata Habari kwa kuandika email yako hapa chini:

LULU AINGIA LOCATION!!!


HATIMAYE staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameingia mzigoni na kufyatua filamu yake mpya baada ya kimya cha muda mrefu, Amani limeinyaka.
Kwa mujibu wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Lulu alitupia picha akiwa ‘location’ kuashiria kwamba amerudi kazini baada ya kusimama kuigiza kwa muda mrefu.
Baadhi ya picha hizo zinamuonesha Lulu akiwa na staa mwingine wa filamu Bongo, Hashimu Kambi mbele ya kamera kwa ajili ya kushuti filamu hiyo ambayo jina lake halijapatikana.
Mara baada ya kutupia picha hizo mtandaoni, watu mbalimbali walimtumia ujumbe kumsifia kwa kumwambia kuwa ana kipaji cha kazi hiyo.
Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo naye alichangia mada hiyo na kumsifu Lulu kwa uwezo wake wa kuigiza. Lulu amekuwa kimya kwa muda mrefu baada ya kupata msala wa kumuua bila ya kukusudia staa mwingine wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba, Aprili 7, mwaka jana, hivi sasa yuko nje kwa dhamana.

0 comments: