RAISI MSAKA KABUMBU NA ANALIPWA MSHIKO WA KUMTOSHA KBSA..!
Nikikupa
nafasi ya kuniambia namba ngapi atakua anacheza huyu president wa nchi
kwenye hili soka unaweza kuotea? hii inaingia kwenye list ya stori kubwa
za millardayo.com
Sasa
unaambiwa club moja huko Bolivia (Sports Boys) imemsajili rais wa
Bolivia Evo Morales kucheza kama kiungo wa kati kuanzia Agosti 2014 na
mgongoni atakua na jezi namba 10 huku mshahara wake kwa mwezi ukiwa ni
dola za Kimarekani 213 kwa mwezi ambazo ni zaidi ya laki 3 za
Kitanzania.
Kwa
sasa mashabiki wanamsubiri president huyo mwenye umri wa miaka 54 ambae
ni shabiki mzuri soka na atakua akiichezea Sports Boys ikiwa ni timu
iliyopo kusini mashariki mwa mkoa wa Santa Cruz.Timu hiyo ambayo ipo katika ligi ndogo imesema rais huyo atakuwa akicheza kwa dakika 20 katika kila mechi watakayokuwa wanacheza hasa ikizingatiwa kuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi.
Rais Morales amewahi kucheza katika mechi nyingi pamoja na wanahabari, viongozi wa umoja na marais wengine huku kumbukumbu ikionyesha mwaka 2007 rais huyo alishiriki katika mechi iliyokusudiwa kupinga kikwazo kilichokuwa kimewekwa kwa Bolivia cha kutoshiriki katika mechi za kimataifa.
Mwaka 2006 alipata matatizo uwanjani kwa kuvunjika mguu wakati alipogongana na kipa.
0 comments: