KAMANDA, ASKARI WAKE LAIVU,ALINASWA GESTI AKIWA NA ASKARI WAKE AMBAYE NI MKE WA MTU..!
KAMANDA
wa kampuni moja ya ulinzi ya jijini Dar es Salaam (jina tunalo), Japhet
Misana ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha mafunzo cha kampuni hiyo,
Alhamisi iliyopita wakati Wakristo wakiwa kwenye hekaheka za Sikukuu ya
Pasaka, alinaswa gesti akiwa na askari wake ambaye ni mke wa mtu.

Kamanda huyo na askari wake (jina tunalo) walijichimbia kwenye gesti hiyo iliyopo Tabata Matumbi, Dar kwenye chumba namba 6.
Ilidaiwa
na chanzo chetu kuwa, kamanda huyo alianza kutokwa na ‘mate’ ya
matamanio kwa askari wake huyo tangu alipofika kwenye kampuni hiyo
kuomba kazi.
Chanzo
hicho kiliendelea kudai kuwa, askari huyo alipewa kazi kwa sharti la
kutoa ‘burudani’ kwa kamanda huyo lakini baada ya kufanikiwa kupata
ajira alianza kumpiga danadana mkubwa wake huyo kuhusu suala la
‘majamboz’ kama walivyokubaliana.

Taarifa
hizo, kwa mujibu wa chanzo, zilimshtua sana mwanaume huyo ambaye
alianza kumwekea mtego mkewe pamoja na bosi wake kwa kumkabidhi kazi
hiyo mdogo wake kuwa ‘shushu’.
Siku
ya Alhamisi Kuu ambayo kimvua kilisumbua karibu jijini zima la Dar
sanjari na kibaridi, shushu huyo alimsikia shemeji yake akizungumza
kwenye simu na mtu mmoja aliyehisiwa kuwa ndiye kamanda wakiahidia
kukutana kwenye gesti hiyo.
Shushushu
huyo haraka alipiga simu kwenye chumba cha Oparesheni Fichua Maovu
(OFM) na kuwaeleza mchezo mzima.Baada ya kupata taarifa hizo bila
kuzubaa, makamanda wa OFM walitumia dakika zisizozidi 10 kutoka makao
makuu ya ofisi zao zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar na kuwasili eneo la
tukio.
OFM
na shushu huyo waliwaona wawili hao wakiongozana na kupiga kona kadhaa
kisha wakaingia kwenye gesti hiyo na kujichimbia kwenye chumba namba
sita.Wawili hao wakiwa chumbani makachero wa OFM waliwasiliana na askari
Polisi wa Kituo cha Tabata ambao nao waliwasili bila kuchelewa.
Walipofika
waliingia ndani ya gesti hiyo na kumtaka mhudumu, walijitambulisha na
kumweleza kilichowaleta pale ambapo mfanyakazi huyo wa mapokezi
alikwenda kuwagongea wateja wake bila kuwaeleza kama arobaini yao
ilitimia.
Kwa
mujibu wa mpelelezi aliyetumwa na mume wa mwanamke huyo, mwanamke ndiye
aliyefungua mlango akiwa na taulo huku kamanda wake akiwa kitandani.
Shushushu
huyo aliongeza kuwa, baada ya kushuhudia tukio hilo alipandwa na jazba
na kutaka kuwapa kipondo lakini polisi walimzuia na kumtia pingu kamanda
huyo hadi kituo cha polisi.
Kamanda
huyo na askari wake walifikishwa kituoni hapo na kuchukuliwa maelezo
ambapo mwanamke huyo aliweka wazi tangu bosi wake huyo alipompa ajira
kwa sharti la kumpa burudani na mengineyo.
Kamanda Misana alifunguliwa kesi ya kudai rushwa ya ngono kwenye jalada lenye namba TBT/RB/2280/2014 na kutupwa rumande.
Kamanda Misana alifunguliwa kesi ya kudai rushwa ya ngono kwenye jalada lenye namba TBT/RB/2280/2014 na kutupwa rumande.
0 comments: