ANGALIA PICHA ZA MKUTANO WA UKAWA MKOANI ARUSHA..!
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (chadema) Dr Wilbrod Slaa akizungumza na wananchi wa Arusha katika viwanja vya Kilombero ikiwa ni mfululizo wa Mikutano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi iliyoanza juzi katika maeneo tofauti ya nchi. Katika mkutano wa Arusha Dr Slaa aliambatana na viongozi wengine kutoka NCCR Mageuzi na Chama Cha Wananchi (CUF) iliyowakilishwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Bw Mustafa Mwanri.
Kutoka kushoto, Bw Elifuraha wa ArushaMambo Radio, Katibu wa Kanda ya Kaskazini Chadema, Mh Amani Golugwa na Dr Slaa
Ulinzi
ulikuwa ni wa uhakika kutoka kwa vikosi vya vyama vyote vitatu. Pichani
ni kijana wa Redbrigade ya Chadema Bw George katika suti maridadi.
Viongozi
mchanganyiko wa vyama vyote vitatu. Katikati anaonekana Dr Slaa akiwa
kulia kwa Mbunge wa Moshi Mjini, Mh Philemon Ndesamburo ambaye
amejitolea Helkopta yake pamoja na gharama za mafuta na rubani kuzunguka
Kanda yote ya Kaskazini hadi Tarime Mkoani Mara.
Dr Slaa akikaribishwa Jukwaani
Mh Ndesamburo akifurahia jambo na mdau wa NCCR
0 comments: