UKAWA WAPATA PIGO..!
'Bunge
Maalumu la Katiba liliridhia azimio la kuzifanyia marekebisho kanuni
zake saba bila kuwapo kwa wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), ambao wamesusia Bunge hilo.
Marekebisho
hayo ya kanuni yanaonekana kuwa pigo kubwa kwa wajumbe hao wa Ukawa kwa
vile sasa hawatapewa tena fursa ya kufafanua maoni ya wachache badala
yake watasoma tu.
Awali,
Kanuni ya 33 ilikuwa ikitaka mwenyekiti wa kamati kutumia muda wa dakika
60 kusoma taarifa yake iliyokuwa ikijumuisha maoni ya wajumbe walio
wengi na taarifa ya wale walio wachache.
Lakini
kanuni hiyo sasa imefanyiwa marekebisho, ambapo mwenyekiti wa kamati
atasoma tu taarifa ya walio wengi na maoni ya walio wachache yatasomwa
na mmoja wa wajumbe wa walio wachache.
Kanuni
hiyo ya 33(5) sasa itasomeka: "Maoni ya wajumbe walio wachache yatasomwa
na mmoja wa wajumbe ambao hawakuunga mkono maoni ya wajumbe walio wengi
kwa muda usiozidi dakika 30."
Akiwasilisha
maelezo ya Kamati ya Maadili na Haki za Bunge, mjumbe wa kamati hiyo,
Evod Mmanda, alisema kuwa hakutakuwa na nafasi tena ya mjumbe kutoka
kundi la wachache kutoa mambo kichwani.
Mmanda
aliyekuwa akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Pandu
Ameir Kificho, alisema maoni ya wachache yaligeuzwa kuwa maoni ya
kisiasa na kubeba hoja za kishabiki za kisiasa. Alisema kuwa kutokana na
marekebisho hayo, hakuna jambo litakalokuwa halijajadiliwa kwenye
kamati, ambalo litaruhusiwa kusomwa na walio wachache ndani ya Bunge
Maalumu la Katiba.
Kanuni
nyingine zilizorekebishwa ni pamoja na ya 32, ambayo sasa inaruhusu
mjumbe yeyote au kundi lolote la wajumbe kupendekeza sura mpya kwenye
Rasimu ya Katiba.
Rasimu iliyowasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ina Sura 17.
Kanuni
nyingine zilizorekebishwa ni 35, 41, 60, 62 na 82 pamoja na sehemu
inayohusu orodha ya yaliyomo katika kanuni hizo za Bunge za mwaka 2014.
Akichangia
hoja ya marekebisho hayo, mjumbe wa Bunge hilo, Anjelina Samike alisema
kwamba wajumbe kutoka kundi la walio wachache walikuwa na maneno magumu
na yasiyo na staha.
Kwa
upande wake, Yusuph Singo alisema nafasi waliyokuwa wakipewa walio
wachache, hawakuitumia kutoa ufafanuzi, badala yake waliitumia kujadili
na kuibua mambo mapya.Baada ya kupitishwa kwa marekebisho hayo, Sitta
alisema kanuni hizo zitaanza kutumika mara moja.
Wajumbe
wanaotokana na Ukawa walisusa kuhudhuria vikao vya Bunge hilo wiki
iliyopita kwa kile walichodai kupinga ukiukwaji wa kanuni na matumzi ya
lugha ya matusi, kejeli na dhihaka.
CHANZO MWANANCHI
0 comments: