China noma,imekusanya hawa watu Uwanja wa Mpira na kuwahukumu kifo..!

Kwa mujibu wa ripoti za shirika la habari la nchi hiyo, Washtakiwa hao ambao walifikishwa mbele ya umati wa takribani watu elfu 7,000 walihukumiwa adhabu mbalimbali huku watatu kati yao wakihukumiwa adhabu ya kifo.

Maafisa wa nchini China wamevishutumu vikundi vya kijeshi vya Uigher ambao ndio sehemu kubwa ya wahalifu hao kwa kusababisha kukua kwa idadi ya mashambulizi katika nchi hiyo.

Picha kutoka katika uwanja huo zimeonyesha magari makubwa ya polisi yakiwa yameegeshwa karibu na kundi kubwa la wahalifu hao kuhakikisha ulinzi wa kutosha huku idadi kubwa ya watu wakishuhudia hukumu hiyo ikitolewa.
0 comments: